Katika ṭaaluma ya fasihi ya kiSwahili uṭeṇḍi maarufu uliyoṭafiṭiwa mno kuhusu masiyala ya nrowa, kazi na majukumu ya mke k̇a mumewe, ni ule wa Ṁanakupona. K̇a mara ya k̇anza, makala haya yanaangaziya uṭeṇḍi ṁengine ambao haujaṭafiṭiwa k̇a ṭafsili wenye kuraṭibu kazi na majukumu ya mume k̇a mkewe. Utendi wa Ramani ya Maisha ya Ndoa (Mume) uliyotungwa na Usṭadh Mahmouḍ Mau unampa mvulana wasiya wa kutumiya katika kufaulisha nrowa yake. Makala haya yaṇjaribu kudhihirisha elimu ya kiḍini na hekima ya ṭajiriba ya kimaisha aliyonayo mtunzi k̇a kumnasihi mvuli kuwa hakuna ukʰuu katika nrowa. Makala haya yakiongozwa na nadhariya ya Usemezano yamechanganuwa maudhui ya hekima ya mtunzi na kubainisha kuwa: k̇enye mukṭadha wa nrowa mke na mume wanasemezana si wao peke yao bali na jamii k̇a ujumla; kuna mabaḍiliko ya maana ya maneno kila kukicha basi na maana ya uume piya inabaḍilika kila kukicha; na ṁishowe, maana inayokuja baaḍa ya kukaa nrani ya maisha ya nrowa huwa ṭafauṭi na ile ilozoweleka. Makala haya yanahiṭimisha kuwa mtunzi aliṭaka kumfunza mvulana na msichana kuwa maisha ya nrowa ni ya watʰu wawili lakini majukumu zaiḍi yanaṁangukiya mume katika kufaulisha nrowa yake. Isiṭoshe, uṭeṇḍi huu unamkazaniya mume amsome mkewe kila siku kila saa ili aweze k̇idhibiṭi nrowa. Naṭija ilopatikana k̇a kuushughulikiya uṭeṇḍi huu ni kubaḍilisha nadhari katika ṭaaluma za kiSwahili na kijinsiya k̇a k̇angaziwa sana Ṁanakupona na kuṭoṭafiṭiwa ṭʰeṇḍi nyenginezo haswa zinazotiliya maanani mtoto wa kiyume.