Chapisho hiki huangalia vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi kwenye Bonde la Ufa la Tanzania, eneo lenye anuwai ya lugha kubwa sana, na lugha kutoka familia za Kibantu, Kikushi, Kiniloti, pamoja na Kisandawe (kinachoweza kuwa na mnasaba na lugha za familia ya Khoi-Kwadi), na lugha kisiwa ya Kihadzabe. Kazi mmoja ya mapema zaidi (Kießling, Roland, Maarten Mous & Derek Nurse. 2007. The Tanzanian Rift Valley area. In Bernd Heine & Derek Nurse (eds.), A linguistic geography of Africa, 186–227. Cambridge: Cambridge University Press) ilivitambua vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi kama sifa bainifu kwenye lugha nyingi za “Eneo la Bonde la Ufa la Tanzania”. Chapisho hiki hutoa taarifa zaidi kuhusu vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi kwenye lugha za eneo hili, pamoja na kuchunguza njia za ukuzaji wa viunzi hivi. Kutokana na uchambuzi huu, picha inayopatikana ni yenye changamani: mipangilio ya matukio hayawezi kuweka Kikushi cha Ufa Magharibi (yaani: West Rift Cushitic) au lugha zake tangulizi kama mtindo kwa ukuzaji pekee wa vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi, na, kwa Kisandawe (na labda lugha za Kidatooga), inaonekana kwamba ukuzaji wa vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi hauwezi hata kuelezwa kama tokeo ya mgusano wa lugha. Kuhusu uwezo wa Bonde la Ufa la Tanzania kuwa “kundi eneo”, chapisho hiki huacha mazungumzo wa jiografia na hoja kwa au dhidi ya “Kundi Eneo la Bonde la Ufa la Tanzania” na huongea zaidi kuhusu matukio moja moja ya kihistoria (linganisha Campbell, Lyle. 2017. Why is it so hard to define a linguistic area? In Raymond Hickey (ed.), The Cambridge handbook of areal linguistics, 19–39. Cambridge: Cambridge University Press) yaliyoweza kusaidia ukuzaji wa vikundi vya viangami vinavyokaa kabla ya kitenzi kwenye lugha sampuli yetu, na vile vile hutumainisha uchunguzi zaidi kwenye historia hizi kwa vifaa vya isimu lakini vile vile za masomo mbalimbali.